NISITIRI Project Campaign

 • Ili mwanafunzi ahudhurie ipasavyo masomo yake anatakiwa ahudhurie siku 194 na vipindi 1740 katika mwaka mmoja wa masomo.
 • Lakini kwa mtoto wa kike hasa wa kijijini amekuwa akikosa masomo kwa wastani wa siku 84 kwa mwaka kutokana na suala la hedhi ambalo ni suala la kimaumbile.
 • Jambo hilo humfanya msichana kukosa kuhudhuria vipindi 756 vyenye Dakika 40 kila kimoja.
 • Hii ni kutokana na changamoto ya kipato cha wazazi wao na pia shule nyingi nchini hasa za vijijini kutokuwa na mazingira rafiki ya usafi kwa wanafunzi wa kike.

Lorna Dadi Foundation kupitia NISITIRI Campaign tunaungana pamoja na serikali, mashirika mbalimbali na jamii kwa ujumla kuhakikisha mtoto wa kike anapata vihifadhi hedhi kwa ajili ya kujisitiri katika mzunguko wake wa mwezi lakini pia anapata elimu na uelewa zaidi kuhusu Hedhi salama.

Lorna Dadi Foundation kwa kushirikiana na mwandishi wa simulizi ya Kiswahili iitwayo “Vipande vya Maisha Vilivyopotea” kupitia NISITIRI Campaign. Asilimia thelathini (30%) ya mauzo ya kila kitabu yatakwenda kusaidia upatikanaji wa vihifadhi hedhi kwa ajili ya mabinti ambao familia zao zina kipato cha chini kisichoweza kuipa hata mlo mmoja kwa siku. Kampeni hii ni ya miezi mitatu ambapo imedhamiria kuchangia kuwapa uhakika wa kusitirika wakati wa hedhi ya kila mwezi kwa kipindi kisichopungua mwaka mzima mabinti 1,000 waliopo katika vijiji vya Matelefu, Igombavanu na Mapogolo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Vitabu vitapatikana

 1. ELITE BOOKSTORE MBEZI BEACH
 2. ELITE BOOKSTORE Quality centre
 3. Review bookshop kariakoo
 4. APE Bookshop MOSHI
 5. KASE STORE Arusha na
 6. Bookpoint Bookshop Arusha.
 7. Mwanza GUNDA BOOKSHOP Bantu street.
 8. MAK Bookshop – Mlimani City, Dar
 9. Ruzinga Bookshop – Bukoba Mjini
0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *