BURUNDI

Mabinti watatu wa miaka 15,16 na 17 walifungwa jela kwa kosa la kuchora-chora picha ya Rais Pierre Nkuruzinza kwenye madaftari yao. Jambo hili lilitafsiriwa na mamlaka ya nchi hiyo kuwa ni kosa  la kumtukana Rais huyo.  Wakili wa mabinti hao amesema hawakuwa na hatia yoyote.

Kufungwa kwa mabinti hao kulivutia watu kutoka pande mbalimbali za Dunia ambapo wanaharakati wa haki za binadamu waliishinikiza serikali ya Burudni kuwaachia huru.