Kuwa wa Tofauti

“Ili uwe tofauti na ulivyokuwa March 2017 ni lazima ufanye vitu vya tofauti au ufanye vitu vilevile lakini katika hali ya utofauti au ufanisi zaidi. Nazungumzia utofauti wenye mwelekeo chanya. Hili jambo tunaambiana kila siku ila wengi wetu wanashindwa kuchukua hatua sahihi.

Wakati Mungu anataka kukupeleka kwenye hatua nyingine mbele ili uweze kutimiza kusudi la maisha yako kuna vitu ni lazima uviache kama vile:

  1. Kuna aina ya watu – yaweza kuwa marafiki au ndugu – ukaribu wenu lazima upungue kama sio kuachana nao kabisa. Hii ni kwa sababu wana influence kubwa kwenye maisha yako na kwa bahati nzuri muda wao wa kuwa karibu na wewe katika kutimiza hatua flani ya kusudi la maisha yako unakuwa umekwisha yaani hawahusiki katika hatua inayofuata ya kutimiza kusudi la maisha yako. Simaanishi uwachukie, hapana, namaanisha fanya jambo sahihi kwa hekima. Mungu anatuamuru tumpende kila lakini hajasema tuwe na urafiki au ukaribu na kila mtu.
  2. Kuna aina flani ya mazingira au niseme aina flani ya maisha inabidi uachane nayo. Maisha ya mazoea ya kufanya jambo fulani mara kwa mara. Kuna mambo ambayo ni kweli tunatakiwa kuyafanya mara kwa mara kwani ni ya muhimu katika kufikia malengo yetu lakini kuna mambo ambayo tunatakiwa kuyafanya katika kipindi fulani kwa ajili ya matokeo yanayohitajika kipindi hicho tu. Sasa mambo ya kufanyika katika kipindi maalumu muda wake unapopita ni lazima tuachane nayo na tusonge mbele ili kuweza kuiendea hatua nyingine kubwa zaidi ya kufikia malengo yetu. Ukitaka kitu kizuri zaidi kitokee katika maisha yako ni lazima ufanye jambo la tofauti lenye tija zaidi. Na kwa kadri unavyoiendea hatua kubwa zaidi ya kutimiza lengo changamoto zinakuwa kubwa zaidi na wakati mwingine inabidi kujitoa zaidi – sacrifice. Huu ni wakati unapojikuta Inakubidi ku-sacrifice vitu fulani fulani ambavyo wewe umekuwa ukiamini kwamba unavihitaji sana au ni vya muhimu sana kwa wakati huo kama vile marafiki wa aina fulani, muda, starehe, nk. Ni lazima ujitoe kwenye; Ukanda wa Faraja, au Ukanda wa Mazoea; aka Comfort Zone kama kweli unataka kufanikisha kusudi la maisha yako.

Baadhi ya Wanafunzi wa Dar Prime Secondary School wakiwa na Matron wao kwenye picha ya pamoja baada ya semina kumalizika

Tuyachukulie Maisha kama mfano wa nyumba anayopewa mtu na mzazi wake. Unapopewa nyumba unapewa na funguo za milango yote. Lakini ufunguo utakaonyeshwa ni ufunguo wa kufungulia mlango mkubwa wa kuingilia ndani. Funguo za vyumbani litakuwa ni jukumu lako kuzibaini ufunguo upi unafungua chumba gani. Na ni lazima ujue kila chumba ndani ya nyumba hiyo kimejengwa kwa ajili ya nini. Na huwezi kujua matumizi ya hivi vyumba kwa wakati mmoja, ila kwa kadri unapokuwa na uhitaji wa dhati wa chumba husika ndipo utajua. Hivi vyumba vinawakilisha matumizi ya nyakati mbalimbali tunazokutana nazo katika maisha. Ni muhimu kuelewa wakati gani unatakiwa kufanya jambo gani. Mzazi wako anapokupeleka shule

anakuwa amekupa ufunguo wa kufungulia mlango mkubwa wa nyumba aliyokupatia. Ni jukumu lako kuzitambua vizuri funguo za vyumba vilivyomo ndani ya nyumba na matumizi ya hivyo vyumba. Tujifunze kuishi maisha sahihi kwa wakati sahihi. Wanaume walikuwepo kabla hatujazaliwa na watakuwepo hata baada ya sisi kufariki, jiulize je ni kweli unahitaji kuwa na boyfriend sasa hivi ukingali bado mwanafunzi?

Kila mtu anapenda kuishi maisha anayoyatamani lakini wenye ujasiri wa kufuata kanuni za mafanikio ni wachache”……….. Ni baadhi ya maneno tu yaliyosikika katika mafundisho tuliyokuwa tukiwapatia mabinti wa shule ya sekondari Dar Prime iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam siku ya 7.5.2017

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *